Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa uboreshaji wa Bandari ya Dar es salaam kupitia kampuni ya DP World umeongeza mapato , idadi ya makasha yanayoingia na kupungua kwa siku ya meli kukaa bandarini.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ameeleza hayo leo Aprili 17,2025 wakati akiongea na Wananchi wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, ikiwa ziara yake ya siku kumi katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Makalla ameeleza hayo akijibu hoja ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche aliyedai kuwa Tanzania imeshindwa kuendesha bandari na kuwapa Watu binafsi.
Makalla amesema Heche hajui mambo ya uchumi na biashara anahitaji aelimishwe faida za uwekezaji na uboreshaji bandari ya Dar es salaam ambayo imekuwa moja ya bandari yenye ufanisi Afrika mashariki na kati
Pia amesema kuwa makaa ya mawe kuuzwa nje ya nchi ni fursa nzuri inayosaidia Serikali na Taifa kwa ujumla kuongeza mapato na fedha za kigeni zinazosaidia kufanya maendeleo ya nchi kutokana na masoko yanayopatikana nje ya nchi.
Leave a Reply