Taarifa Kamili inayohusu Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025/2026 Kupitia Ajira Portal hii ni orodha na list ya majina kwenye PDF walioajiriwa 2025 na vituo vyao vya kazi. Majina ya walimu waliopata kazi 2025 Walioitwa Kazini Walimu Kada Za Ualimu.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza rasmi majina ya walimu waliopata ajira kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Tangazo hili linahusu waombaji wote wa nafasi za ualimu waliopitia mchakato wa usaili kati ya tarehe 14 Agosti 2024 hadi 17 Januari 2025. Wale waliokuwa katika kanzidata ya awali pia wamejumuishwa endapo nafasi za kazi zimepatikana.
Majina ya walimu waliopata kazi yamewekwa kwenye PDF inayopatikana kupitia Ajira Portal, na pia yanaonyesha vituo vyao vya kazi walikopangiwa.
Maelezo Muhimu Kuhusu Walimu Walioitwa Kazini
Kipengele | Maelezo |
---|---|
Kipindi cha Usaili | 14 Agosti 2024 hadi 17 Januari 2025 |
Waliofaulu | Waombaji waliopitia usaili na wale waliokuwepo kwenye kanzidata waliopangiwa kazi baada ya nafasi kupatikana |
Mahali pa Kuchukua Barua | Ofisi za Sekretarieti ya Ajira – UDOM, Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro |
Muda wa Kuchukua Barua | Ndani ya siku 7 kuanzia tarehe ya tangazo |
Nyaraka za Kuja Nazo | Vyeti halisi vya masomo (kuanzia kidato cha nne) kwa ajili ya uhakiki |
Kitambulisho Kinachokubalika | Kitambulisho cha Taifa, Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Kitambulisho cha mpiga kura au leseni ya udereva |
Kituo cha Kuripoti Kazi | Katika ofisi ya mwajiri iliyotajwa kwenye barua |
Waliokosa Majina | Wamekosa nafasi kwa sasa lakini wanahimizwa kuomba tena kwenye nafasi zitakazotangazwa mbeleni |
Taarifa Zaidi | Tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira: www.ajira.go.tz |
Maelekezo kwa Walioitwa Kazini
Waombaji waliotajwa katika orodha ya walioajiriwa wanapaswa kuchukua barua za kupangiwa vituo vya kazi ndani ya siku saba. Baada ya muda huo kupita, barua ambazo hazitachukuliwa zitatumwa kwa anuani za Posta za waombaji husika.
Baada ya kuchukua barua, mwalimu atatakiwa kuripoti kwa mwajiri wake akiwa na vyeti halisi kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kupokea barua ya ajira rasmi.
Nyaraka Muhimu za Kuambatanisha Wakati wa Kuripoti
Unapokwenda kuripoti kituoni, hakikisha umebeba nyaraka zifuatazo:
- Cheti cha kuzaliwa
- Vyeti vya masomo (Form IV, VI, Stashahada au Shahada)
- Kitambulisho cha taifa au kingine kinachotambulika
- Barua ya kupangiwa kituo kutoka Ajira Portal
- Cheti cha usajili kutoka TSC (baraza la walimu)
Wito kwa Walioikosa Nafasi
Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana kwenye tangazo, ni vyema kutambua kuwa kwa wakati huu hawakufanikiwa katika usaili. Hii haina maana ya mwisho wa safari; mnaombwa kufuatilia matangazo yajayo na kuendelea kuwasilisha maombi yenu kwani nafasi mpya hutangazwa mara kwa mara.
Kupata Orodha Kamili ya Majina
Orodha kamili ya majina ya walimu waliopangiwa kazi pamoja na vituo vya kazi inapatikana kupitia PDF inayopatikana kwenye tovuti ya Ajira. Unaweza kupakua kupitia kiungo kifuatacho:
List Ya Majina Kamili:
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 02-04-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 27-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 25-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 22-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU 20-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU 18-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU 17-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 14-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 13-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 12-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 10-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 06-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 04-03-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 02-02-2025
Bofya hapa kuona majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025 (PDF)
Mwisho Kabisa
Uteuzi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha idadi ya walimu inakidhi mahitaji ya shule za umma. Sekretarieti ya Ajira inawataka walimu wote walioteuliwa kuwa wazalendo, waadilifu, na wazingatie maadili ya kazi zao wanapoanza utekelezaji wa majukumu yao mapya.
Kwa maswali au ufafanuzi zaidi, tembelea ofisi za Sekretarieti ya Ajira au tembelea tovuti rasmi ya www.ajira.go.tz.
Imetolewa na: Katibu – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Makala Nyingine:
Matangazo Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 2025/2026
Leave a Reply