Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelitaka Jeshi la Magereza, Mamlaka husika na vyombo vya dola kutoa taarifa wazi na za haraka kwa umma kuhusu mahali alipopelekwa Tundu Lissu wakisema wamepewa taarifa kuwa gerezani hayupo.
Taarifa iliyotolewa leo Aprili 18, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia imesema “Leo ljumaa, Aprili 18, 2025, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Wakili Ali Ibrahim Juma, Mawakili, Familia na Wanachama kwa nyakati tofauti, wamefika katika Gereza la Keko ambapo Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Tundu Lissu anashikiliwa”
“Hata hivyo, juhudi zao za kumuona Lissu hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa hayupo katika gereza hilo, cha kusikitisha, hawakupewa maelezo yoyote rasmi juu ya alipopelekwa”
“CHADEMA tunalitaka Jeshi la Magereza, mamlaka husika na vyombo vya dola kutoa taarifa wazi na za haraka kwa umma kuhusu mahali alipopelekwa , Tundu Lissu, iwapp bado anashikiliwa katika Gereza la Keko, ni haki ya familia, viongozi na wanachama kumuona ni haki ya msingi ya kibinadamu na kikatiba”
Makala Nyingine:
ACT; Uchukuaji Fomu Uraisi, Ubunge Muda Waongezwa
Leave a Reply