Mwili Wa Carina (Hawa) Wawasili Kuzikwa Kesho Kisutu

Mwili wa Mwigizaji Hawa Hussein Ibrahim ( Carina) umepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ukitokea Nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kwenda mwezi mmoja uliopita kutokana na matatizo ya tumbo.

Carina ambaye ni Mama wa Mtoto mmoja, alianza kuugua miaka tisa iliyopita na kufanyiwa upasuaji wa tumbo mara nane katika Hospitali tofauti Nchini Tanzania na sasa baada ya mwili wake kuwasili Dar es salaam, anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho katika makaburi ya kisutu.

Makala Nyingine:

Polisi Yaonya Vurugu Kisutu kwa Lissu

CHADEMA Yahoji alikopelekwa LISSU

ACT; Uchukuaji Fomu Urais, Ubunge Muda Waongezwa