Anyimwa Mafao ya Mil 224 Kisa Kaiba Elfu 18

Mwanaume mmoja Nchini Japan ambaye amefanya kazi ya Udereva wa Mabasi kwa kuwa takriban miaka 29, amepoteza mafao yake ya kustaafu yenye thamani ya dola 84,000 za Kimarekani ( zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 224 ) baada ya kufukuzwa kazi kwa kosa la kuiba dola 7 ( sawa na shilingi 18,800) kutoka kwa Abiria.

Imeelezwa kuwa tukio hili lilitokea kwenye basi la Jiji la Kyoto alilokuwa akiliendesha ambapo kupitia camera ya usalama alionekana akipokea fedha kutoka kwa Abiria na kuzitia mfukoni badala ya kuziingiza kwenye mashine ya ukusanyaji wa nauli.

Dereva huyo mwenye umri wa miaka 58 alikanusha shtaka hilo alipohojiwa na Wakubwa wake licha ya ushahidi wa video kuwepo na Mahakama ya awali ilimuunga mkono na kusema adhabu ya kupoteza mafao yote ilikuwa kali mno lakini kesi hiyo ilipanda hadi Mahakama Kuu ya Japan na hivi karibuni Mahakama Kuu imetoa uamuzi wa mwisho kwa kuunga mkono uamuzi wa awali wa Jiji la Kyoto na hivyo kupigilia msumari wa moto kuwa Dereva huyo hana haki ya kulipwa mafao yake ya kustaafu.

Aidha Maafisa wa usafiri wa umma wa Kyoto wamesema uamuzi huo ni wa kupongezwa wakisisitiza kuwa Madereva wote wanahusika na fedha za umma na hufanya kazi wakiwa peke yao hivyo nidhamu ni ya lazima vilevile walisema endapo hatua kali zisingechukuliwa lingekuwa ni fundisho baya kwa wengine na lingeweza kudhoofisha imani ya umma kwa Taasisi hiyo ya usafiri.

Makala Nyingine:

Mwili Wa Carina (Hawa) Wawasili Kuzikwa Kesho Kisutu

Ni JUX na Priscilla JP2025 From Lagos

DK Kikwete Awasilisha Ujumbe wa SSH Kwa Traore