Ally Kamwe Apigwa Faini Ya Mil.5

Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza maamuzi ya Kamati ya Maadili ya TFF ambayo iliwaita watu kadhaa wa familia ya michezo wakiwemo Ahmed Ally wa Simba SC na Ally Kamwe wa Yanga SC.

Ally Kamwe, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, alishtakiwa na Kamati ya
Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la Mwaka 2021.

Baada ya kusikiliza pande zote na kupitia nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake, Kamati imemtia hatiani kwa kosa aliloshtakiwa nalo na kumpa adhabu ya kulipa faini ya sh. 5,000,000 (milioni tano) na onyo la kutofanya kosa la kimaadili ndani ya kipindi cha miaka miwili. Adhabu hiyo inaanza tarehe 16/04/2025.

Habari Nyingine:

Azam Fc Yaiomba Nafasi Ya Kimataifa: Mchakato Mgumu Ulio Mbele Yao