Ahmed Ally Hana Hatia Ushahidi Haujatosha

Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza maamuzi ya Kamati ya Maadili ya TFF ambayo iliwaita watu kadhaa wa familia ya michezo wakiwemo Ahmed Ally wa Simba SC na Ally Kamwe wa Yanga SC.

Ahmed Ally, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, alishtakiwa na klabu ya Yanga akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la Mwaka 2021.

Baada ya kupitia maelezo ya pande zote husika pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake, Kamati ilibaini kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumuingiza hatiani kwa kosa aliloshtakiwa nalo na imemuachia huru.

Habari Nyingine:

Ally Kamwe Apigwa Faini Ya Mil.5

Azam Fc Yaiomba Nafasi Ya Kimataifa: Mchakato Mgumu Ulio Mbele Yao