Hashim Lundenga Wa Miss TZ Afariki

Jina lake lilitajwa sana kwenye mashindano ya Miss Tanzania kwa miaka mingi kutokana na uwepo wake kwenye mashindano hayo akitumikia nafasi yake kwa nguvu zote kama Mratibu.

Familia yake imesema Hashim Lundenga amefariki leo akiwa Hospitali Jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda wa miaka minne “Ni kweli Hashim Lundenga amefariki leo Hospitalini, alikuwa anasumbuliwa na stroke ambayo ilimletea magonjwa mengi sana”

“Ameumwa kwa muda wa miaka minne, msiba upo Bunju B, kuhusu taratibu za mazishi bado hatujakaa, tutatoa taarifa baadae kuhusu maziko”

Habari Nyingine:

Wasira; Hatuwezi Kukubali Amani ivurugwe

Mwili Wa Carina (Hawa) Wawasili Kuzikwa Kesho Kisutu

Simba VS Stellenbosch Utaitazama Supersport

Ajari ya gari la Kamba Yaua Wanne ITALIA