CHADEMA: Tundu Lissu Amehamishiwa Ukonga

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema leo April 19, 2025, Viongozi wakuu wa Chama hicho wamekutana na uongozi wa Jeshi la Magereza na kufahamishwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amehamishiwa katika Gereza la Ukonga.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, imesema “Kufuatia taarifa hiyo, Familia, Wanachama wa CHADEMA na Watanzania wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu mahali alipo Mheshimiwa Lissu, wanataarifiwa kuwa sasa wanaweza kumtembelea kwa kufuata taratibu za kawaida za kumuona mahabusu katika Gereza hilo”

“Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, Mheshimiwa John Heche, anatarajiwa kufika Gereza la Ukonga leo kwa ajili ya kumwona Mheshimiwa Tundu Lissu na kuzungumza naye kuhusu hali yake”

Habari Nyingine:

CHADEMA Yahoji alikopelekwa LISSU

Polisi Yaonya Vurugu Kisutu kwa Lissu

Wasira; Hatuwezi Kukubali Amani ivurugwe

ACT; Uchukuaji Fomu Urais, Ubunge Muda Waongezwa