Nafasi 50 za Madereva (Madereva 50) – Unique Consultancy Services Co. LTD, Kampuni ya Unique Consultancy Services Co. LTD inatangaza nafasi hamsini (50) za kazi kwa madereva wa magari mbalimbali katika maeneo ya miradi ya kampuni yaliyoko Tanga, Kagera, Geita na Tabora.
Aina za magari yanayohitajika kuendeshwa ni pamoja na:
- Matrekta
- Mabasi makubwa
- Mabasi madogo
- Magari ya mizigo (Pick-up)
- Magari ya kubeba maji (Water Bowsers)
- Malori ya mafuta (Fuel Tanks)
- Malori ya mizigo (Trucks)
- Mitambo ya kuinulia mizigo (Cranes)
Sifa za Mwombaji
- Awe anaelewa vizuri sheria za usalama barabarani na awe na uwezo wa kuzifasiri.
- Awe na umri usiopungua miaka 25 na usiozidi miaka 45.
- Awe na leseni halali ya daraja linalostahiki kuendesha chombo husika, ambayo haijaisha muda wake.
- Awe amehudhuria mafunzo ya VETA au chuo kinachotambuliwa na serikali na kupata cheti.
- Awe tayari kwenda kufanya kazi katika maeneo ya miradi. Chakula na malazi vitapatikana bure.
Jinsi ya Kuomba
Waombaji wote wanatakiwa kutuma maombi yao kwa barua pepe ifuatayo:
uccjobs2025@gmail.com
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 Juni, 2025.
Tafadhali ambatanisha CV yako pamoja na vyeti vingine muhimu katika muundo wa PDF katika barua pepe hiyo.
Tangazo hili linawahusu madereva wa viwango mbalimbali – jiunge nasi kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa nchini!
Nafasi Nyingine za Kazi:
Leave a Reply