Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 10 Septemba, 2024 hadi tarehe 24 Februari, 2025, kuwa matokeo ya usaili huo yako tayari na majina ya waliofaulu yameorodheshwa kwenye tangazo hili.
Orodha hiyo pia inajumuisha baadhi ya waombaji waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
MAELEKEZO MUHIMU KWA WALIOFAULU USAILI
Barua za kupangiwa vituo vya kazi
Waombaji wote waliopangiwa vituo vya kazi watapata barua zao kupitia akaunti zao za Ajira Portal, sehemu ya “My Applications”. Wanaelekezwa kupakua (download) na kuchapisha (print) barua hizo kwa ajili ya kuziwasilisha wanaporipoti kazini.
Kuripoti kazini
Wote waliopangiwa vituo vya kazi wanapaswa kuripoti kwa Mwajiri ndani ya muda uliowekwa katika barua za kupangiwa kazi wakiwa na vyeti halisi vya taaluma, kuanzia kidato cha nne na kuendelea, kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua rasmi ya ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili
Wanatakiwa kufahamu kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili. Hivyo, wanahimizwa kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi nyingine zitakapotangazwa na Sekretarieti ya Ajira.
Kwa taarifa zaidi na kuangalia orodha kamili ya walioitwa kazini, tafadhali tembelea tovuti ya Ajira Portal kupitia kiunganishi:
PDF ya majina Hapa Chini;
TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 24-04-2025
Imetolewa na:
Katibu, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Tarehe: 24 Aprili, 2025
Makala Nyingine:
Matangazo Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 2025/2026
Matangazo Ya Walimu Walioitwa Kazini 2025/2026 Kupitia Ajira Portal
Leave a Reply