Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 24-04-2025 hadi 08-05-2025. Hatimaye, waombaji kazi watakaofaulu usaili huo watapangiwa vituo vya kazi.
Waombaji kazi walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
Maelekezo ya Usaili:
Tarehe na Muda wa Usaili:
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 24-04-2025 hadi 08-05-2025. Muda na sehemu ya usaili imeainishwa kwa kila kada.
Vitu vya Kuleta kwa Usaili:
Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa (Mask).
Kitambulisho cha Utambulisho:
Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho cha utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
- Kitambulisho cha Mkazi
- Kitambulisho cha Mpiga kura
- Kitambulisho cha kazi
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya kusafiria
- Leseni ya Udereva
- Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji
Vyeti Halisi:
Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha kuzaliwa, Kidato cha IV, Kidato cha VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na vyeti vingine kulingana na sifa za mwombaji.
Vyeti Visivyokubalika:
Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, au hatiza matokeo za Kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWI NA HAUTARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
Gharama za Usaili:
Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi wakati wa usaili.
Tarehe, Muda na Mahali pa Usaili:
Kila msailiwa azingatie tarehe, muda, na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
Waombaji wa Nje ya Tanzania:
Kwa waombaji kazi waliosoma nje ya Tanzania, wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA).
Waombaji Kazi Wasioonekana Kwenye Orodha:
Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili wanatambua kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
Kada Zinazohitaji Usajili wa Kitaaluma:
Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma, wanapaswa kuja na vyeti vyao halisi vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi.
Namba ya Mtihani:
Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani, kwa kuwa namba hizo hazitatolewa wakati wa usaili.
Mabadiliko ya Jina:
Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
List Ya Majina Kwenye PDF
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA (NECTA) MAJINA YA NYONGEZA 18-04-2025
Makala Nyingine:
Leave a Reply