Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kuongeza muda wa kuchukua fomu ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar kuanzia April 18,2025 hadi May 25, 2025, Ubunge Viti Maalum, Uwakilishi na Uwakilishi Viti Maalum kuanzia April 18,2025 hadi May 31, 2025 na Udiwani na Udiwani Viti Maalum kuanzia April 18,2025 hadi May 25, 2025.
Taarifa iliyotolewa leo April 18,2025 na Katibu Mkuu wa ACT, Ado Shaibu imesema “Kamati ya Uongozi Taifa ya ACT kwenye kikao chake cha April 15, 2025 ilitoa maelekezo kwa Ofisi ya Katibu Mkuu kuongeza muda wa Wanachama kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais wa Zanzibar, Ubunge, Ubunge wa Viti Maalum, Uwakilishi, Uwakilishi wa Viti Maalum, Udiwani na Udiwani wa Viti Maalum ili kutoa fursa ya kutosha kwa wanachama kugombea, ninayo furaha kuwajulisha Wanachzma wa ACT Wazalendo na Wananachi kwa ujumla kuwa muda wa kuchukua fomu za kugombea nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais wa Zanzibar, Ubunge, Ubunge wa Viti Maalum, Uwakilishi, Uwakilishi wa Viti Maalum, Udiwani na@Udiwani wa Viti Maalum umeongezwa”
“Katika utekelezaji wa agizo la kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Feb 23, 2025, Ofisi ya Katibu Mkuu ilitoa maelekezo ya kuruhusu wanachama kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali, licha ya maelekezo hayo kutolewa kabla ya tamko rasmi la Chama cha ACT Wazalendo kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu 2025, Wanachama wetu wengi wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali”
“Mathalani, kwa nafasi za Ubunge, jumla ya Wanachama 317 wamechukua fomu hadi sasa, kwa nafasi ya uwakilishi, jumla ya Wanachama 106 wamejitokeza kuchukua fomu, tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Wanachama wetu waliojitokeza kuchukua fomu, kuchukua kwao fomu kabla ya Chama kutangaza ushiriki kwenye uchaguzi ni ishara ya wazi ya utayari wao katika mapambano ya kulinda na kutetea thamani ya kura”
Makala Nyingine:
Leave a Reply