Ajari ya gari la Kamba Yaua Wanne ITALIA

Watu wanne wamefariki na mmoja kujeruhiwa baada ya Gari la kamba linalofahamika kama ( cable car ) kuanguka katika Mlima Monte Faito Nchini Italia baada ya kamba inayotumika kulisafirisha na kulishikilia gari hilo kukatika ghafla.

Miongoni mwa waliopoteza maisha ni Mfanyakazi wa Gari hilo, Watalii wawili kutoka Uingereza na mmoja kutoka Israel huku Mtalii mwingine wa Kiyahudi ambaye yupo katika hali mbaya akiendelea kupatiwa matibabu kutokana na kupata majeraha makubwa.

Kwa upande mwingine Maafisa wa Uokoaji wamefanikiwa kulishusha na kutoa msaada kwa Gari jingine la kamba lililokwama hewani likiwa na Abiria 16 ambapo Vyombo vya Habari Italia vimesema ajali hiyo sio ya kwanza kwani mwaka 2021 gari hilo lilipata ajali na kuua Watu 14 Nchini humo.

Habari Nyingine:

Anyimwa Mafao ya Mil 224 Kisa Kaiba Elfu 18

Mwili Wa Carina (Hawa) Wawasili Kuzikwa Kesho Kisutu

Wasira; Hatuwezi Kukubali Amani ivurugwe