Waziri wa Kililmo Hussein Bashe ametoa muda wa siku saba kwa nchi za Malawi na Afrika Kusini endapo hazitabadilisha msimamo wa kuzuia mazao na bidhaa za Kilimo ya kutoka Tanzania kwenda kwenye nchi zao,Serikali ya Tanzania itazuia uingizwaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka nchi hizo mbili au kupitisha mazao kwenye nchi zingine.
Bashe amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wanaotekekelza Miradi ya kuwezesha Vijana na Wanawake katika sekta ya Kilimo
“Hatujawahi kumsumbua jirani yeyote lakini majirani marajingi wakiwa na njaa na shida wako mlangoni kwetu wakishainuka kidogo wanazuia mazao yetu kuingia kwenye nchi zao” Hussein Bashe Waziri wa Kilimo
“Nimetoa notisi leo by Jumatano wasipofungua Malawi na South Afrika kutufungulia kupeleke mazao yetu ya kilimo kama yanavyoingia ya kwao kwetu hatutazuia zao lolote la kwao kuingia Tanzania vilevile sitawaruhusu Malawi na wenzake kupitisha kile kinachohusiana na mmea wa kilimo kuingia wala kupita Ontransit kwenye nchi hii” Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.
Makala Nyigine:
Leave a Reply