DK Kikwete Awasilisha Ujumbe wa SSH Kwa Traore

Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehitimisha ziara yake kwa kukutana na Rais wa Burkina Faso, Captain Ibrahim Traoré.

Mkutano huo umefanyika Jijini Ouagadougou leo Aprili 17, 2025 na kuhudhuriwa na Maafisa waandamizi kutoka Serikali zote mbili akiwemo Balozi Hoyce Temu.

Katika mkutano huo, Dkt. Kikwete ameelezea shukrani zake kwa kupata fursa ya kukutana na Captain Traoré na kumkabidhi ujumbe maalum wa Rais Samia.

“Rais wangu amenituma nije kuwasilisha Ujumbe Maalum kwako na nimefurahi umenipa fursa hiyo na leo umeupokea rasmi”

Dkt. Kikwete amewasilisha pia salamu za Rais Samia kuhusu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Afrika, hususan kubadilishana uzoefu ili kwa pamoja Afrika iweze kuendeleza rasilimali zake kwa faida ya Watu wa bara lao.

Makala Nyingine;

Uwekezaji wa DP world Umeongeza Mapato

Bashe Atoa siku 7 kwa Malawi na Afrika Kusini