Jokate Aongoza Matembezi Ya First Time Voters

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Jokate Mwegelo ameongoza matembezi ya Maelfu ya Vijana ambao pia ni Wapiga Kura wapya katika uchaguzi mkuu mwaka huu 2025 (Samia First Time Voters), ambapo matembezi hayo yameishia Katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es salaam panapofanyika kongamano uzinduzi wa Samia First Time Voters.

Jokate ameongoza matembezi ya Vijana hao leo Aprili 19,2025 Jijini Dar es Salaam ambapo kwa pamoja wamefika kwa wingi katika uzinduzi huo wa programu Maalum ya Vijana hao kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu ambapo Jumuiya hiyo imesema imeweka mikakati mbalimbali itakayofanikisha ushindi wa Rais wa Tanzania Dk.Samia kupitia kundi la Vijana wa Tanzania.

Kongamano hilo limehudhuriwa na Vijana mbalimbali wakiongozwa na Umoja wa Vijana CCM Seneti Ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Dar es salaam, na Wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo KM Jokate ndiye Mgeni rasmi.

Samia First Time Voters hii ni kampeni mahususi yenye lengo la kuhamasisha na Kuelimisha kundi la Vijana waliotimiza umri wa miaka 18 hivi karibuni na kupata sifa ya kuwa Wapiga kura Kwa mara ya kwanza katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025, kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

Habari Nyingine:

Jeshi la SADC Congo Kuja TZ Kupitia Rwanda

Hashim Lundenga Wa Miss TZ Afariki

Ally Kamwe Apigwa Faini Ya Mil.5

CHADEMA Yahoji alikopelekwa LISSU