Tangazo La Kuitwa Kazini Benki Kuu Ya Tanzania (BOT) 17-04-2025

Tangazo La Kuitwa Kazini Benki Kuu Ya Tanzania (BOT) 17-04-2025, Orodha ya Majina walioitwa kwenda kazini.

Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote waliofanya usaili wa mahojiano tarehe 21, 24 na 25 Machi, 2025 kuwa majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Aidha ajira zao zitakuwa rasmi pale vyeti vyao vitakapohakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika.

Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kufika Benki Kuu ya Tanzania Makao Makuu Ndogo Dar es Salaam tarehe 23 Aprili, 2025 Saa Mbili na Nusu Asubuhi ili kukamilisha taratibu mbalimbali za Ajira, wakiwa na nyaraka zilizoainishwa katika tangazo hili kwa uhakiki.

Nyaraka za kuwasilisha kwa ajili ya uhakiki ni;

  1. Vyeti halisi (Original Certificates) kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na vyeti vingine (kutegemeana na nafasi uliyokuwa umeomba), na nakala mbili zilizothibitishwa na mwanasheria,
  2. Nakala mbili za Kitambulisho cha Taifa (NIDA) zilizothibitishwa na mwanasheria,
  • Picha ndogo mbili za rangi (passport size photograph).

MAJINA YA WALIOFAULU NA KUCHAGULIWA KATIKA KADA MBALIMBALI

TANGAZO LA KUITWA KAZINI.pdf

Makala Nyingine:

Matangazo Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 2025/2026

Matangazo Ya Walimu Walioitwa Kazini 2025/2026 Kupitia Ajira Portal

Matangazo ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Na Ajira Portal 2025