Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limekuwa likifuatilia matamko mbalimbali na mipango ya baadhi ya Viongozi wa Chama cha CHADEMA kikihamasisha Watu kukusanyika April 24, 2025 eneo la Mahakama ya Kisutu huku katika mipango yake kikilenga kufanya vurugu kwa lengo la kushinikiza mamlaka za kisheria kumwachia mmoja wa mtuhumiwa Tundu Lissu atakayepelekwa siku hiyo Mahakamani hapo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro kwenye taaarifa aliyoitoa leo April 17,2025 amesema “Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawakumbusha Wahusika kuwa Mahakama ni Mamlaka za kisheria zilizo huru na hazipaswi kutishwa au kuingiliwa wakati wa utekelezaji wa majukumu yake”
“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, linawatahadharisha Watu wote wanaohamasisha kuhusiana na nia hiyo ovu kutoshiriki kwenye mpango huo na linatoa onyo kali kuwa wale wote wanaopanga na ambao watajaribu kutekeleza kinachohamasishwa watashughulikiwa vikali sana lakini kwa mujibu wa sheria za nchi”
Makala Nyingine:
Leave a Reply