Makamu Menyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira, amesema ni vema Wananchi wakafahamu kwamba katika amani ndani yake kuna haki, hivyo Chama kitaendelea kuihubiri kuhakikisha inapatikana haki.
Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Tabora, jana, Wasira amesema kuna Watu wanahoji CCM inazungumzia sana amani lakini haizungumzii haki, huku akibainisha kuwa wanaotoa madai hayo ni Watu wazito.
“Sasa nikasema ngoja niende (Tabora) kwenye kitovu ambapo Mwalimu Julius Nyerere alitoa machozi kwa ajili ya amani, tuwasaidie kuelewa kwamba ukizungumza amani ndani ya amani kuna haki kwa sababu amani ikikosekana wenye uwezo mdogo wanaumia”
“Amani ikikosekana Wanawake na Watoto wao katika nchi jirani wanakilimbilia Tabora…ukilinda amani unalinda haki tena unalinda haki ya wanyonge, unalinda haki ya wasiokuwa na sauti”
“Unazungumza haki ya Mtu anasema anataka kuwa Rais halafu anaambiwa eti tukibadili Katiba anakuwa Rais na haki inayosemwa ni Mtu mmoja badala ya kuzungumza haki ya walio wengi, tunauliza huyo anayesema hatuzungumzi haki tunazungumza amani sijui anadhani ndani ya amani hakuna haki”
Makala Nyingine;
Polisi Yaonya Vurugu Kisutu kwa Lissu
Leave a Reply